Nyakati za mavuno zimewadia huko Silicon Valley. Majengo ya Ofisi yaliyo kwenye muelekeo wa Barabara Kuu ya 101 yamesheheni ofisi za kampuni mbalimbali. Gharama ya kupangisha nyumba imepanda, huku mahitaji ya maeneo ya kifahari ya kujivinjari kwenye miji ya kitalii kama vile Ziwa Tahoe, yakiwa ndiyo ishara kamili ya malimbikizi ya mali. Eneo hilo la ghuba lilikuwa ndio kitovu cha kuanzishwa kwa viwanda vya bidhaa za kununurisha umeme pamoja makampuni ya kompyuta na tovuti ambayo hatimaye yamekua na kufikia upeo wa juu. Wataalamu wake wabunifu waliandaa programu kabambe zilizoufanya ulimwengu kuonekana kuwa na mustakabali mzuri, kuanzia kwa simu maizi za rununu zenye viwambo vya mguso hadi kwa usakuraji wa moja kwa moja wa maktaba za kilimwengu mpaka kwa ubunifu wa kiwango cha kuelekeza droni kutoka umbali wa maelfu ya maili. Ufufuliwaji wa shughuli zake za kibiashara mnamo 2010 ilikuwa ishara tosha kwamba mchakato huo unaendelea vizuri.
Kwa hivyo, inaweza kuwashangaza kuwa baadhi ya watu huko Silicon Valley wanafikiria kwamba eneo hilo limekuwa kama bangwa, na kwamba kiwango cha ubunifu kimedorora kwa miongo kadhaa iliyopita. Peter Thiel, mwanzilishi wa Paypal na mwekezaji wa kwanza wa nje katika Facebook, anasema kwamba ubunifu huko Marekani “uko kati ya hali mahututi na kifo’’. Wahandisi kwenye sekta na fani zote wametamauka kwa hisia sawa. Hata hivyo, kikundi kidogo kinachokua cha wachumi wanatambua athari ya kiuchumi ya ubunifu wa kisasa labda unaweza kufifisha ulinganifu wa hali ilivyo sasa na ilivyokuwa awali.
[ … ]
Sehemu nyingi zimeanzisha ubunifu unaotekelezwa kwa kutumia kawi iliyochakatwa. Kompyuta zimeanza kuelewa lugha asilia. Watu wanathibiti michezo ya video kupitia kwa miondoko ya viwiliwili pekee — teknolojia ambayo kwa siku za usoni itapata mashiko na matumizi yake katika ulimwengu wa kibiashara. Uchapishaji wa kipimo cha upandeolwa una uwezo wa kutoa vitu vya aina mbalimbali, na hivi karibuni vinaweza kushughulikia tishu za wanadamu pamoja na bidhaa nyinginezo za kikaboni.
Mbunifu wa kutia shaka anayeweza kupuuza suala hili na kulichukulia kama “ahadi zisizotimilika”. Lakini wazo la ukuaji unaowezeshwa na teknolojia ni lazima liendelezwe bila kupingwa ama ukuaji huo upungue kabisa, badala ya kutoka na kumiminika, itakuwa inakinzana na historia. Chad Syverson wa Chuo Kikuu cha Chicago anaelezea kwamba ukuaji wa uzalishaji wakati wa enzi za uvumbuzi wa umeme ulikuwa wa madongemadonge. Ukuaji huo ulikuwa wa polepole sana wakati wa kipindi muhimu cha uvumbuzi wa ubunifu wa umeme katika mwisho wa karne ya 19 na mwanzo wa karne ya 20; kisha ukaongezeka.